Ijumaa 30 Oktoba 2026 - 03:00
Shambulio dhidi ya Soko na Kituo cha Mafuta cha Al-Jawf ni Uhalifu wa Kivita na Uhalifu dhidi ya Binadamu

Hawza/ Shirika la Kitaifa la Haki za Binadamu la Yemen limelaani kwa maneno makali zaidi uhalifu wa kutisha uliofanywa leo na Saudi Arabia inayoishambulia Yemen katika mkoa wa Al-Jawf. Limesema kuwa shambulio la makusudi na la moja kwa moja dhidi ya Soko la Al-Hazm na Kituo cha Mafuta cha Al-Taysir, katika mkoa wa Al-Jawf, limesababisha vifo vya raia 14 na kujeruhiwa watu 16, wakiwemo wanawake watatu na watoto kadhaa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Shirika la Kitaifa la Haki za Binadamu la Yemen limelaani kwa maneno makali zaidi uhalifu wa kutisha na wa kutisha mno uliofanywa leo na Saudi Arabia inayoishambulia Yemen, kwa kulenga kwa makusudi na moja kwa moja Soko la Al-Hazm na Kituo cha Mafuta cha Al-Taysir katika mkoa wa Al-Jawf.

Mashambulizi hayo ya kikatili yamesababisha idadi ya awali ya wahanga kufikia mashahidi 14 na majeruhi 16. Miongoni mwa majeruhi hao wamo wanawake watatu na watoto kadhaa, waliokuwa sehemu ya wanunuzi wasio na hatia na raia waliokuwa wakitekeleza shughuli zao za kila siku. Hali hiyo imeibua tukio la umwagaji damu linalotikisa dhamiri za binadamu na kumshtua kila mwenye moyo wa utu.

Shirika hilo limesisitiza kuwa mauaji haya ni uhalifu kamili wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, pamoja na kuwa ukiukaji wa wazi wa mikataba na desturi zote za kimataifa na uvunjaji wa kanuni za sheria ya kimataifa ya kibinadamu, ikiwemo kanuni za kutofautisha malengo ya kijeshi na raia, uwiano wa nguvu zinazotumika na kuchukua tahadhari. Kanuni hizo zinakataza kabisa kulenga masoko ya umma na miundombinu ya kiraia.

Shirika la Haki za Binadamu limebainisha kuwa kulipuliwa kwa makusudi soko lililojaa wanunuzi na kituo cha mafuta cha kiraia wakati wa mapambazuko, pamoja na mauaji ya wanawake na watoto, kunafichua sura halisi ya uchokozi wa Saudi Arabia kama mashine ya mauaji isiyosita kumwaga damu ya wananchi wa Yemen.

Aidha, shirika hilo limeeleza kuwa kuendelea ukimya wenye mashaka wa Umoja wa Mataifa, pamoja na ushirikiano wa kimyakimya wa jumuiya ya kimataifa na taasisi zake, ndiko kunakoitia moyo Saudi Arabia kuendelea kung’ang’ania kufanya mauaji zaidi dhidi ya wananchi wa Yemen.

Shirika la Haki za Binadamu la Yemen limeutaja Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza la Haki za Binadamu kuwa vinabeba wajibu kamili wa kisheria na kimaadili kuhusiana na uhalifu huu.

Shirika hilo limetaka makamanda wa Saudi Arabia wanaohusika na uchokozi huo wafuatiliwe na wawajibishwe kama wahalifu wa kivita mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, likisisitiza kuwa hawapaswi kuruhusiwa kukwepa adhabu.

Vilevile, shirika hilo limetaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuwalinda raia na miundombinu ya kiraia, na kusitishwa uhalifu wa mauaji ya kimbari unaotekelezwa kwa utaratibu dhidi ya wananchi wa Yemen.

Mwisho, Shirika la Haki za Binadamu la Yemen limesisitiza kuwa; damu ya mashahidi waliouawa katika Soko la Al-Hazm, mkoani Al-Jawf—wawe wanawake, watoto au wanaume—haitapotea bure kadiri muda unavyopita. Damu hiyo itaendelea kuwa laana dhidi ya wauaji na wahalifu, na itabaki kuwa kilio kitakachosikika mbele ya ulimwengu wa kinafiki, kikitaka mauaji ya wananchi wa Yemen yasitishwe.

Mchambuzi mashuhuri wa Yemen ameeleza:
Nafasi ya maulamaa wa Saudi Arabia katika kueneza vurugu na mazingira ya chuki dhidi ya Iran

Hawza/ Mabadiliko ya msimamo wa Saudi Arabia kuhusu Iran yameelekeza upya macho ya watu kwenye nafasi ya makundi ya kidini ya nchi hiyo katika miaka iliyopita; makundi hayo hayo yaliyotumia lugha ya kimadhehebu kugeuza tofauti za kisiasa na Tehran kuwa uadui wa kidini, ambao matokeo yake yalidhihirika katika mapigano ya kikanda, hususan nchini Yemen.

Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Mohsen Ali Al-Jamal, mwanaharakati wa vyombo vya habari kutoka Yemen, amekosoa misimamo ya maulamaa wa kutoa fatwa wa Saudi Arabia katika makala yake.

Baadhi ya maulamaa wa kutoa na wahubiri wa Saudi Arabia, kupitia fatwa na propaganda zao dhidi ya Iran, walilihusisha jina la Iran na tuhuma kama vile “Majusi”, na kuupa uadui dhidi ya Tehran sura ya kidini. Hata hivyo, leo hii, Saudi Arabia inapokaa pamoja na Iran kwenye meza ya mazungumzo, swali zito linajitokeza: Tuhuma zote zile na juhudi za kuumba uadui ziliishia wapi?

Kwa miaka mingi, watu walikuwa wakishawishiwa kuamini kwamba tofauti na Iran ilikuwa imevuka mipaka ya ushindani wa kisiasa na kufikia kiwango cha mkinzano wa kiitikadi. Hii ilikuwa ni simulizi iliyowasilisha mazungumzo na Tehran, badala ya kuwa chaguo la kisiasa, kana kwamba ni jambo lisilopatana na imani za kidini. Hata hivyo, sasa Saudi Arabia ileile iliyokuwa na nafasi katika kujenga mazingira ya chuki dhidi ya Iran, inafuata njia ya kushirikiana na Iran.

Mabadiliko haya ya mwelekeo yanazidisha uzito wa maswali kuhusu nafasi ya baadhi ya maulamaa wa kutoa fatwa na wahubiri wa Saudi Arabia; watu ambao, kwa kutumia lugha ya kimadhehebu, waliunganisha tofauti za kisiasa na mpasuko wa kidini, na kuchangia kuundwa kwa mazingira ambayo ndani yake uadui dhidi ya Iran haukuwasilishwa kama msimamo wa kisiasa, bali kama wajibu wa kiitikadi.

Matokeo ya mazingira ya aina hiyo hayakuishia tu katika uhusiano kati ya Tehran na Riyadh. Hata nchini Yemen, kaulimbiu za kimadhehebu ziligeuka kuwa msingi wa kuzidisha tofauti na kuwavuta vijana wa kusini kuingia vitani dhidi ya wananchi wenzao. Vijana hao walilipa gharama ya mapigano hayo kwa maisha yao, huku familia zao zikibaki katika majonzi ya kuwapoteza wapendwa wao.

Leo hii, maslahi ya kisiasa yanapokuwa mbele na njia ya mazungumzo inapofunguliwa, swali hili bado linabaki: Ikiwa kushirikiana na Iran kunawezekana, kwa nini kwa miaka mingi Iran ilizungumziwa kwa lugha ya tuhuma na chuki?

Serikali zinaweza kubadilisha misimamo yao kadiri hali inavyobadilika; lakini athari za propaganda za kimadhehebu haziwezi kufutika kwa urahisi hivyo kutoka katika akili na maisha ya watu. Makovu ya vita, familia zilizofiwa na mipasuko iliyojitokeza kati ya jamii mbalimbali haviwezi kutoweka kwa kubadilika tu kwa lugha ya kisiasa.

Mkanganyiko uliopo kati ya kaulimbiu za jana na mazungumzo ya leo unaonesha umuhimu wa kupitia upya simulizi zilizogeuza tofauti za kisiasa kuwa uadui wa kidini. Simulizi hizo hatimaye ziliwalazimisha wananchi wa kawaida kulipa gharama ya ushindani ambao leo hii, wale waliokuwa watoa maamuzi wanaweza kuchagua njia nyingine.

Chanzo: Afaq News Yemen

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha